Tarehe Iliyotumwa 2022-11-15 18:06:48
Makabidhiano ya Muongozo wa Ufundishaji Elimu ya Afya ya Uzazi, Ukimwi na Stadi za Maisha
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR IMESEMA KUWEPO KWA MUONGOZO WA UFUNDISHAJI ELIMU YA AFYA YA UZAZI, UKIMWI NA STADI ZA MAISHA ITAWASAIDIA WANAFUNZI KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA UDHALILISHAI NA MIMBA ZA UMRI MDOGO.
AKIZUNGUMZA KATIKA HAFLA YA MAKABIDHIANO YA MUONGOZO HUO KATIKA UKUMBI WA KITUO CHA WALIMU BUBUBU NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMLI ZANZIBAR MH ALI ABDULGULAM HUSSEIN AMESEMA MUONGOZO NI NJIA MOJA WAPO YA KUWAKINGA WATOTO NA VITENDO VYOTE VITAKAVYOWAHARIBIA MUSTAKABALI WA MAISHA YAO.
NAE MKURUGENZI WA TAASISI YA ELIMU YA ZANZIBAR NDUGU ABDALLA MOHAMED MUSSA AMEIOMBA UNESCO KUISAIDIA SERIKALI KATIKA KUANDAA VITABU KWA MUJIBU WA LUGHA AMBAYO ITAWASAIDIA WATOTO.
WAKATI HUO HUO NDUGU MATIAS HERMAN KUTOKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA ELIMU SAYANSI NA UTAMADUNI UNESCO AMESEMA MUONGOZO ITAWASAIDIA WALIMU WALIMO SKULI PAMOJA NA WAVYUONI ILI KUWAJENGEA MAARIFA KWA WATOTO KULINGANA NA UMRI WAO BILA YA KUATHIRI UTAMADUNI WA KIZANZIBAR.
Tarehe Iliyotumwa 2022-10-26 08:25:01
Uandaaji wa Kamusi ya Lugha ya Alama la Kielektroniki
WADAU WA UANDAAJI WA KAMUSI LA LUGHA YA ALAMA LA KIELECTRONIC WAMESHAURIWA KUTUMIA MANENO YANAYOENDANA NA TAMADUNI ZA KIZANZIBARI ILI YAWEZE KUTUMIKA SEHEMU YOYOTE. MENEJA UTAWALA NA RASILIMALI WATU KUTOKA TAASISI YA ELIMU ZANZIBAR MUSSA HASSAN ZYMA AMEELEZA HAYO KWA NIABA YA MKURUGENZI WA TAASISI HIYO ALIPOKUWA AKIFUNGUA WARSHA YA SIKU TATU YA KUANDAA MUUNDO WAKAMUSI LA LUGHA YA ALAMA LA KIELECTRONIC HUKO KITUO CHA WALIMU KIEMBE SAMAKI. AMESEMA MATUMIZI MAZURI YA LUGHA HIYO ITAWAWEZESHA WALENGWA KUWAFIKIA UJUMBE KWA URAHISI BILA YA KUWA NA UKAKASI AU UGUMU WA ALAMA ZINAZOTUMIKA. AMEFAHAMISHA KUWA SERIKALI IMEAMUA KUANDAA KAMUSI HILO ILI KUHAKIKISHA KUWA SUALA LA LUGHA YA ALAMA KATIKA ELIMU LIMEZINGATIWA KWA KILA MTU. KWA UPANDE WAKE MKUU WA DIVISHENI YA UKUZAJI MITAALA YA MAFUNZO YA UALIMU NA URATIBU WA SEKONDARI MWANA ALI ABDALLA AMESEMA LENGO LA KUSHIRIKISHWA WADAU HAO NI KUPATA TAALUMA NA UFANISI UTAKAOSAIDIA KATIKA UTAYARISHAJI WA KAMUSI HIYO YA KIELEKRONIK. NAO WASHIRIKI WA WARSHA HIYO WAMEIOMBA TAASISI YA ELIMU KUANGALIA MAZINGIRA HALISI JUU YA MUUNDO WA KAMUSI HILO KWA KUHUSISHA LUGHA ZISIZO PUNGUA TATU KWA MUJIBU WA WATUMIAJI WAKE.
Tarehe Iliyotumwa 2022-10-15 16:31:17
Warsha ya uchukuaji wa maoni ya uandaaji wa kamusi la lugha ya alama la kielektroniki
Taasisi ya Elimu ya Zanzibar (TEZ) inajukumu la kuandaa mtaala na kuhakikisha vifaa vya kujifunzia na kufundishia vinapati kana kwa wanafunzi wote hadi wenye mahitaji maalum. Hayo ameyasema Mkuu wa Divisheni ya Ukuzaji mitaala ya Mafunzo ya Ualimu na Uratibu wa Sekondari Bi Mwana Ali Abdallah kutoka Taasisi hiyo wakati akifungua warsha ya uandaaji wa kamusi la kielektroniki la lugha ya alama katika ukumbi wa kituo Cha walimu Kiembe samaki Mjini Unguja. Amesema katika mtaala mpya wanafunzi wenye mahitaji maalum wamezingatiwa , hivyo taasisi imeona ipo haja ya kuwa na kamusi la kielektroniki lenye kutumia lugha ya alama . Aidha amesema kamusi la lugha ya alama linalo andaliwa litaendana na mabadiliko ya teknolojia litakalo muwezesha mwanafunzi kupata ujuzi zaidi wa lugha ya alama. Pia amewaomba washiriki wa warsha hiyo kuhakikisha wanatanguliza uzalendo kwa kuona mawazo yao yata saidia kutatua changamoto zilizomo katika misamiati na alama muhimu zinazohitajika kuingizwa katika Kamusi hilo. Kwa upande wao washiriki wa warsha hiyo wameishukuru Wizara ya Elimu Zanzibar kupitia Taasisi ya Elimu kwa kupata mahirikiano makubwa kwaajili ya kutoa maoni ili kupunguza changamoto zinazo wapata wanafunzi wenye mahitaji maalum kwani nao watapata taaluma sawa na wanafunzi wengine. Warsha hiyo ya siku mbili imewashirikisha wadau kutoka Jumuia ya Wakalimani Zanzibar, Chama cha viziwi , umoja wa watu wenye ulemavu, wakufunzi kutoka Chuo cha Kiislamu Zanzibar na chuo cha Archibishop Tabora Tanzania Bara.
Tarehe Iliyotumwa 2022-07-16 11:56:02
Uchukuaji wa maoni kwa walimu juu ya uimarishaji wa viwango vya kujifunza
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Mwanakhamis Adam Ameir , akifungua warsha ya Uchukuaji wa maoni kwa walimu juu ya uimarishaji wa viwango vya kujifunza(achievement standards) vya Elimu ya Maandalizi na Msingi Hafla ilio fanyika katika ukumbi wa kituo cha Walimu cha Michakaini Pemba.