Warsha ya kuandaa Mfumo wa upimaji wa ' Large Scale Assessment'

Naibu Katibu Mkuu Taalauma wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Mwanakhamis Adam Ameir amefungua Warsha ya Siku tano ya kuandaa Mfumo wa upimaji wa ' Large Scale Assessment' kwa ajili ya kupima uwezo wa wanafunzi wa darasa la nne na kidato cha pili katika masomo ya Kiswahili, English na Hisabati. Warsha hiyo imewashirikisha wakuza mitaala kutoka Taasisi ya Elimu ya Zanzibar na maafisa mitihani kutoka Baraza la Mitihani la Zanzibar chini ya usimamizi wa washauri elekezi kutoka kampuni ya NFER ya nchini Uingereza.

Huduma Tunazotoa

Huduma zinazotolewa na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar.

Mitaala

Kuishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya mambo yanayohusiana na ukuzaji Mitaala ya Elimu ya Maandalizi, Msingi, Elimu ya Sekondari pamoja na Vyuo vya Ualimu

Tafiti

Kufanya tafiti za Elimu na Kuthibiti Ubora kwenye vifaa vya kufundishia na kujifunzia

Vifaa vya Kufundishia

Kuratibu Utayarishaji wa Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia kwa walimu na wanafunzi

Kutoa Mafunzo

Kutoa Mafunzo kazini yanayohusiana na Mitaala na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia

Viongozi Wetu

23Miaka

Ya uzoefu katika kutoa huduma ya Mitaala

6657Walimu

Jumla ya walimu waliopatiwa
mafunzo ya mitaala

7760Walimu

Tunategemea kuwapatia mafunzo
ya Mtaala mpya 2024

1,222,756
Vitabu vya Mwalimu na Mwanafunzi

Vimeshapishwa kwa ajili
ya mtaala mpya 2024