Tarehe Iliyotumwa 2023-02-26 15:44:41
Mafunzo ya Upitiaji wa vitabu katika mtaala mpya
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Elimu ya Zanzibar mwalim Abdalla Mohammed Mussa amewataka wadau watakaoshiriki katika kazi ya upitiaji wa vitabu vipya vya maandalizi na msingi kuwa makini katika kazi hiyo ili kuepusha makosa madogo madogo yatakayosababisha kurejesha nyuma juhudi za Serikali. Mwalim Abdalla ametoa wito huo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu ya kutathmini miswada ya vitabu vya kiada na viongozi vya mwalim kwa wadau hao yanayofanyika katika skuli ya Dk Shein Rahaleo. Amesema lengo la kutolewa mafunzo hayo ni kuhakikisha vitabu vitakapoanza kutumika vinakuwa na ubora zaidi na kuepusha makosa kulingana na walengwa husika na mazingira halisi ya Zanzibar. Mkurugenzi Abdalla katika hafla hiyo alitumia fursa ya kuwapongeza wadau mbalimbali ambao walishiriki katika uandaaji wa vitabu hivyo kuanzia mwanzo hadi hatua iliyofikia. Kwa upande wake Meneja Idara ya Utafiti na Udhibit Ubora kutoka Taasisi ya Elimu ya Zanzibar Nd Faridu Muhammed Wakil amesema mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuhakisha vitabu hivyo vinakuwa Bora zaidi kwa watumiaji . Mkufunzi wa mafunzo hayo ambae ni mhariri kutoka shirika la Oxford Frederik Silvester amesema katika kuvipitia vitabu hivyo washiriki hao watambue kuwa vitabu hivyo vinakwenda kuwaandaa wataalamu wa baadae. Miswada ambayo inatarajiwa kupitiwa baada ya mafunzo hayo ni mswada wa vitabu vya darasa la maandalizi mwaka wa kwanza darasa la kwanza, la nne na la saba Mafunzo hayo yameandaliwa na Taasisi ya Elimu ya Zanzibar kupitia Idara ya Utafiti na Udhibiti ubora.
Tarehe Iliyotumwa 2023-02-07 13:44:41
Walimu wa darasa la kwanza wapatiwa mafunzo ya Mtaala mpya - Pemba
Walimu wanaofundisha Darasa la Kwanza wametakiwa kuzingatia malengo ya ufundishaji ili kuwaandaa wanafunzi kiumahiri. Wito huo umetolewa na Mkaguzi Mkuu wa Elimu Bi Maimuna Fadhil Abas katika ukumbi wa Kituo cha Walimu Michakaini wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya utekelezaji wa mtaala mpya yaliyowashirikisha walimu wanaofundisha Darasa la kwanza. Bi Maimuna amesema mtaala mpya nahitaji kujituma hivyo nivyema walimu kuangalia malengo ili waweze kufundisha kwa Ufanisi kulingana na malengo ya Mtaala huo. Pia Bi Maimuna amewataka Walimu kuhusisha masomo na mazingira ya nyumbani ya mwanafunzi ili kuwawezesha wanafunzi hao waweze kutumia taaluma katika mazingira yao. Wakati huo huo Mkaguzi Mkuu wa Elimu ametoa pongezi kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kupitia Taasisi ya Elimu kwa kuona haja ya kufanya mafunzo yatakayowajengea walimu uwezo wa kutekeleza Mtaala huo. Nae Mratibu Taasisi ya Elimu Bi Asha Soud Nassor amesema lengo la Mafunzo hayo nikuwapatia Walimu Uelewa wa utekelezaji wa mtaala mpya unaolenga kumuandaa mwanafunzi kiumahiri. Aidha amesema kubadilika kwa Mtaala kunatokana na Kutokea kwa Mabadiliko katika Ulimwengu pamoja na mahitaji ya ya kijamii hivyo mtaala huo umetokana na kufikia muda wa mabadiliko kisheria na kimahitaji ya jamii husika. Nae mshiriki wa mafunzo hayo Asaa Rashid Ali akitoa neno la shukran kwa Mkaguzi Mkuu wa Elimu mara baada ya kufungua mafunzo hayo ameahidi kwamba watayafanyia kazi mafunzo watakayoyapata ili waweze kufikia ufanisi uliokusudiwa. Taasisi ya Elimu Zanzibar inaendelea kutoa mafunzo kwa wadau mbali mbali wa elimu ili kuhakikisha kwamba mtaala unaolenga kumuandaa mwanafunzi kiumahiri unatekelezwa kwa ufanisi.
Tarehe Iliyotumwa 2023-02-07 13:13:10
Walimu wa darasa la kwanza wapatiwa mafunzo ya Mtaala mpya - Unguja
Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali mh Lela Muhammed Mussa amewataka walimu kufanya kazi zao kwa uwadilifu ili lengo la Serikali la kuwa na wataalam Bora wa baadae liweze kufikiwa. Mh Lela ameeleza hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya mtaala mpya kwa walimu wanaofundisha darasa la kwanza huko kituo cha walimu Bububu. Amesema dhamira ya Serikali ya kuandaa mtaala mpya ni kuhakikisha wanafunzi wanapomaliza ngazi ya msingi wanakuwa wanaujuzi kulingana na mazingira halisi ya Zanzibar. Mh Lela amefahamisha kuwa uwajibikaji wa walimu ndio njia pekee ya kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa. Akigusia suala la udhalilishaji mh Lela amewataka walimu kuwa makini na watoto ili kuwaepusha na majanga hayo ambayo kwasasa yamekuwa ni hatari kwa jamii Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu ya Zanzibar ndg Abdalla Mohammed Mussa amesema malengo ya kutolewa mafuunzo hayo ni kuwaandaa walimu kwenda kutekeleza vyema mtaala huo. Mwalimu Abdalla amesema hitakuwa Jambo la busara kwa walimu kupokea mafunzo hayo na baadae kutoyafanyia kazi katika sehemu zao za kazi. Mafunzo ya mtaala mpya kwa walimu yanafanyika kwa muda wa siku tano katika vituo vyote vya walimu Unguja na Pemba.
Tarehe Iliyotumwa 2023-01-17 09:11:47
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR IMEWATAKA WALIMU WA MAANDALIZI KUACHA KUFANYAKAZI KWA MAZOWEA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR IMEWATAKA WALIMU WA MAANDALIZI KUACHA KUFANYAKAZI KWA MAZOWEA ILI KUSAIDIA JUHUDI ZA SERIKALI KUINUA HADHI YA ELIMU YA ZANZIBAR. NAIBU WAZIRI WA WIZARA HIYO MH ALI ABDULGULAM HUSSEIN AMEELEZA HAYO ALIPOKUWA AKIFUNGUA MAFUNZO YA MTAALA MPYA KWA WALIMU WA MAANDALIZI MWAKA WA KWANZA KANDA YA PEMBA HUKO SKULI YA MICHAKAINI WILAYA YA CHAKE CHAKE KUSINI PEMBA AMESEMA IWAPO WALIMU WATATUMIA VIZURI MTAALA MPYA WA UJENZI WA UMAHIRI WATAWEZA KUISAIDIA SERIKALI KATIKA KUFIKIA MALENGO YAKE. AMESEMA LENGO LA SERIKALI NI KUHAKIKISHA KUWA WATOTO WOTE WANAPATA ELIMU AMBAYO ITAWEZA KUIBUWA VIPAJI VYAO KUANZIA NGAZI YA MAANDALIZI KWA KUTUMIA MTAALA HUO MPYA. KWA UPANDE WAKE KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR ND KHAMIS ABDALLAH SAID AMEWASISITIZA WALIMU KUFUNDISHA KWA VITENDO ZAIDI WANAPOKUWA DARASANI NA NJE YA DARASA. AMESEMA MTAALA HUO NI MPYA HIVYO JUHUDI ZA WALIMU KATIKA KUFUNDISHA ZINAHITAJIKA IKIWEMO MICHEZO YA KITOTO AMBAYO NAYO IMO KATIKA MTAALA HUO. WASHIRIKI WA MAFUNZO HAYO WAMESIFU HATUA YA SERIKALI KWA KUWASHIRIKISHA WALIMU WA SKULI BINAFSI KATIKA KUWAPATIA ELIMU HIYO YA MTAALA MPYA AMBAYO NI CHACHU YA KUWAJENGA UMAHIRI WANAFUNZI WA ZANZIBAR. WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI KUPITIA TAASISI YA ELIMU YA ZANZIBAR IPO KATIKA HATUA YA KUTOA ELIMU JUU YA MTAALA MPYA KWA WALIMU WANAOFUNDISHA NGAZI YA MAANDALIZI MWAKA WA KWANZA UNGUJA NA PEMBA.